Tanzania yaadhimisha miaka 61 ya Uhuru
9 Desemba 2022Matangazo
Tanganyika ambayo mwaka mmoja baada ya Uhuru ilitangazwa kuwa Jamhuri, ilijiunga na iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar mwaka 1964 kuunda taifa jipya la Tanzania.
Hii leo sherehe ambazo kwa kawaida hupamba maadhimisho ya siku ya Uhuru zimefutwa, baada ya rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan kuamuru fedha zilizotengwa kwa ajili ya dhifa na maonesho ya kijeshi zitumike kujenga mabweni ya shule za wasichana.
Gharama zilizokuwa zimepangwa kutumika ni dola 445,000.
Uamuzi kama huo wa kuzifuta sherehe za uhuru uliwahi pia kuchukuliwa mwaka 2015 na baadae mwaka 2020 chini ya utawala wa rais wa zamani hayati John Pombe Magufuli.