Teknolojia rafiki yajadiliwa Davos
20 Januari 2023Mawaziri wa biashara kutoka mataifa mbalimbali wametangaza mpango wa kukuza sera za biashara zinazounga mkono hatua za kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa. Tangazo hilo linajiri katika siku ya tano na ya mwisho ya Kongamano la Kiuchumi la Dunia mjini Davos.
Wakizungumza na waandishi wa habari mawaziri hao wamesema malengo yao ni pamoja na kuhakikisha ufikiaji bora wa kimataifa wa teknolojia rafiki na kukuza bidhaa ambazo zinazingatia malengo ya hali ya hewa na uendelevu.
soma 2023: Uchumi unatarajiwa kuimarika
Waziri anayehusika na uzalishaji, biashara, uwekezaji na uvuvi nchini Ecuador Julio Jose Prado ameelezea umuhimu wa majadiliano juu ya kuoanisha sera za biashara na malengo ya hali ya hewa.
Huku viongozi wengi wa Ulaya wakihofia sheria ya nishati safi Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte amesema dunia inapaswa kufurahia kwamba Marekani inashughulikia suala la mabadiko hali ya hewa.
Sheria ya Kupunguza Mfumko wa Bei ya Marekani
Kutokana na Sheria ya Kupunguza Mfumuko wa Bei ya Marekani Kuna hofu kwamba makampuni ya Ulaya yatatolewa nje ya soko la Marekani na kunyimwa uwekezaji wa teknolojia ya kijani.
Seneta wa Marekani Joe Manchin amesema sheria hiyo haina nia ya kuwaumiza washirika lakini inalenga kupata teknolojia safi ili kuongeza kasi.
Baadhi ya waliohudhuria Kongamano la Kiuchumi la Dunia mwaka huu wamesema kuwa maendeleo mazuri ya uchumi wa China yana umuhimu mkubwa kwa dunia, na wameeleza matumaini yao kuhusu ukuaji wa uchumi wa China katika mwaka huu mpya.
Hii ni baada ya naibu waziri mkuu wa China Liu He kusema kwamba Beijing itaendelea kufanya uwekezaji wa kigeni na itaimarisha ushirikiano wa kimataifa.
soma Guterres:Tuwajibike ili kuwa na dunia salama
Akizungumza katika mahojiano na kituo cha Televisheni cha China, Jeremy Jurgens, mkurugenzi mkuu wa Kongamano hilo, amesema ukuaji wa uchumi wa China ni muhimu ili kupunguza shinikizo la uchumi wa dunia unaodorora na kwamba China ina mchango mkubwa katika sekta ya viwanda na ugavi duniani.
"China kurejea katika uchumi kutasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa shinikizo hilo la kushuka kwa uchumi. Natarajia China bado itachukua jukumu muhimu sana hapa. Ikiwa unafikiria mchango ambao China ilitoa katika ufumbuzi wa hali ya juu wa nishati, kwa mfano, katika nishati ya jua. Uwezo wa uzalishaji, sola nyingi za bei ya chini ambazo tunapata leo ni matokeo ya kuongezwa kwa uwezo wa utengenezaji ambao ulifanyika nchini China."
Ushirikiano huu unaongozwa na mawaziri wa biashara kutoka Ecuador. Umoja wa Ulaya, Kenya na New Zealand na zaidi ya mataifa 50 yamejiunga mpango huo.
//AP