1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Kenya 2022: Yanayojiri mjini Kisumu

Zainab Aziz Mhariri: Babu Abdalla
11 Agosti 2022

Baada ya ngoja ngoja ya muda mrefu, hatimaye matokeo ya kura ya uchaguzi mkuu katika nyadhifa mbali mbali yameanza kutangazwa huku vituo vilivyosalia vikitarajiwa kufuata mkondo huo hii leo Alhamisi.

https://p.dw.com/p/4FOTz
Kenia Wahlen 2022
Picha: Brian Ongoro/AFP

Shangwe na nderemo zimetanda katika baadhi ya maeneo jimboni Kisumu, Siaya na Vihiga baada ya baadhi ya wagombea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu kutangazwa washindi na maafisa wasimamizi katika ngazi ya maeneo bunge. Katika nafasi ambazo zimetangazwa washindi ni pamoja na nafasi za uwakilishi wadi na ubunge na tayari katika nyakati za usiku wa giza washindi waliojawa na furaha walipata fursa ya kutoa shukrani zao.

Wafuasi wa mgombea wa urais Raila Odinga pichani katika jimbo la Kisumu
Wafuasi wa mgombea wa urais Raila Odinga pichani katika jimbo la Kisumu Picha: AP

Washindi waliotangazwa sasa wanajiunga na msururu wa wengine katika maeneo mengine ya bunge jimboni Kisumu hasa maeneo ya Nyano, Seme, Ugunja, ila maeneo yaliyosalia kukamilisha hesabu hadi tukienda hewani ni Kisumu Magharibi na Mashariki.

Mwandishi wa DW Musa Naviye alizungumza pia na mwandishi wa habari anayefuatilia zoezi la kuhesabu kura jimboni Siaya Elphus Guya ambaye amesema baadhi ya maeneo ambayo washindi wametangazwa ni wabunge kwa mfano mbunge wa alego Samuel Atandi na wawakilishi wadi. Huko Vihiga nimezungumza naye Martin Ombima mwandishi wa habari, anasema hali sio tofauti na maeneo mengine, ananipa mfano wa mbunge wa Vihiga Earnest Kagesi wa chama cha ANC cha Kenya Kwanza ambaye ametetea kiti chake sawia na wawakilishi wadi katika bunge la jimbo la Vihiga.

Wafuasi wa wagombea katika jimbo la Kisumu
Wafuasi wa wagombea katika jimbo la KisumuPicha: Brian Ongoro/AFP

Kuhusu mrengo unaovuma jimboni humo anasema mbivu na mbichi itabainika kufikia leo asubuhi ila tathmini ya sasa ni kwamba muungano wa Azimio umetwaa nafasi za wawakilishi wadi 12 kumi kati yao wakiwa wa chama cha ODM huku wenzao wa Kenya Kwanza wakipata viti 8 na viti 7 vya chama cha ANC. Zoezi la kuhesabu ya kura ngazi ya maeneo bunge kinatazamiwa kukamilika Alhamisi 11.08.2022 na kufuatiwa na hesabu katika kituo kikuu cha ujumlishaji kura maeneo ya kaunti.

Mwandishi: Musa Naviye