Namna Trump alivyobadili sera ya kigeni duniani
24 Oktoba 2020Kuanzia mwanzoni mwa kampeni zake za 2016, Donald Trump aliweka wazi malengo ya sera yake ya kigeni kwa kutumia maneno mawili tu:"Amerika kwanza."
Na sasa, baada ya karibu miaka minne ya urais wa Trump, maneno hayo yametanuliwa kwa ukweli na matukio. Uchukuaji wa hatua za upande mmoja na makabiliano ndiyo hatua zilizopamba sera ya kigeni ya Trump, kama ilivyokuwa kwa ubadilishaji wa watumishi serikalini, matukio yenye kushangaza na ya kutatanisha.
Soma pia: Mdahalo wa mwisho: Trump na Biden walumbana juu ya COVID -19
Bila kujali matokeo ya uchaguzi wa rais wa Marekani Novemba 3, mabdiliko chini ya Trump katika maudhui ya sera na utekelezaji vimeunda uwanja ambamo watendaji wengine wa dunia wanaendesha diplomasia, pamoja na mikakati yao wenyewe. Haya ni baadhi ya mabadiliko makubwa:
Kuepuka uhusishaji wa mataifa mengi
Tangu kuingia madarakani, Trump amepuuza ushirikiano wa kimataifa. Siku tatu baada ya kuanza muhula wake, aliiondoa Marekani kutoka ushirkiano wa kanda ya Atlantiki, ambao ni makubaliano ya kibiashara na mataifa ya Asia. Baadae aliiondoa Marekani kutoka mikataba na mashirika kadhaa ya kimataifa, kama vile Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na Mkataba Tabianchi wa uliofikiwa 2015 mjini Paris.
Zaidi ya hayo, hatua ya ukuaji wa Marekani mara nyingi imekuwa ya upande mmoja, bila kujali muafaka wa kimataifa, kama vile uamuzi wa kuutambua rasmi mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel na kuhamishia ubalozi wake mjini humo.
Soma pia: Trump: Sudan kuondolewa kwenye orodha ya wafadhili wa makundi ya kigaidi
Margaret MacMilan, profesa wa historia katika vyuo vikuu vya Toronto na Oxford na mwanahistoria wa kigeni katika Baraza la Masuala ya Nje, alisema "kwa kweli Marekani imeharibu kile kilichokuwa mtandoa wa manufaa wa ushirikiano na taasisi za kimataifa za mtandao huo. Nadhani imefanya nafasi ya Marekani duniani kuwa dhaifu zaidi."
Mnamo mwezi Septemba, utafiti kutoka taasisi ya Pew ulionyesha kuwa kiwango cha kukubalika kwa Marekani miongoni mwa mtifa mengi kimeshuka kwa hali ya chini kabisaa kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miongo kadhaa.
Uhusiano wa kanda ya Atlantiki umeharibiwa
Uhasama wa Trump kuelekea ushirika wa mataifa unawakalisha tofauti ya kifalsafa kati ya Washington na miji mkuu ya Ulaya," iliandika taasisi ya amani ya kimaita ya Carnegie katika tathmini yake Februari 2020 juu ya uhusiano wa mataifa ya kanda ya Atlantiki, ushirikiano kati ya Ulaya na Marekani ambao ulijitokeza baada ya Vita Kuu vya pili vya Dunia, na unawakilisha maadili ya pamoja, malengo na mikakati ya kidunia.
Soma pia: Salman amwambia Trump suala la Palestina litatuliwe kwa haki
Lakini mpasuko kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani chini Trump ni zaidi ya mgawiko wa kiitikadi tu; Trump amelaumu kwa nguvu na kukomesha uhusiano wa kanda ya Atlantiki. Amehiji mara kwa mara maadili ya miungano kama NATO, akatangaza uondoaji wa adhabu wa vikosi vya Marekani kutoka Ujerumani, kuanzisha ushuru wa biashara dhidi ya Umoja wa Ulaya na kutishia vikwazo kuhusiana na bomba la gesi la Urusi la Nord Stream 2.
MacMillan anaamini mashaka hayo yanaweza kusababisha mabadiliko ya yatakayodumu muda mrefu. "Ni kama urafiki. Unaweza kuwaamini marafiki zako, na imani hiyo inapovunjika, ni vigumu kuirejesha," alisema. "Ulaya ilikuwa imejenga mazowea ya kumtegemea kaka mkubwa mjini Washington. Na pengine hivi sasa Waulaya wanasema hatuwezi kufanya hivyo na tunapaswa kujenga - kama tulivyozungumza kila wakati kwa miongo - kuendeleza zaidi sera yetu ya nje."
China yatiwa katika wakati mgumu
Kuanzia vita vya kibiashara vilivyosababishwa na ushuru wa kulipizana kisasi hadi shinikizo la Marekani kwa mataifa mengine kuifungia kampuni ya China ya Huawei kwenye ujenzi wa mtandao wa mawasiliano ya G5, msimamo wa makabiliano wa Trump dhidi ya China umeilaazimu nchi hiyo ya Asia kuangaziwa kimataifa.
Soma pia: HRW: Marekani yamuwekea vikwazo Bensouda
Ukosoaji mkali umekaribishwa na wengi wanaoamini kwamba China umenufaika isivyo haki kutokana na utaratibu wa kimataifa wa kibiashara kwa muda mrenfu sana, huku wakati huo huo ikitenda ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.
"Rais amekuwa sahihi kuikabili China kuhusu matendo yake katik nyanja ya biashara," aliandika Richard Haass, rais wa Baraza la Mambo ya Nje, katika dibaji ya tathmini ya katikati mwa muhula ya sera ya kigeni ya Trump.
MacMillan ana mtazamano sawa. "Sitaki kumpa sifa Trump kwa mengi, lakini nadhani yumkini alikuwa sahihi kukosoa - au utawala wake ulikuwa sahihi kuikosoa China kuhusu mali za kisomi," alisema. Wakati mzozo wa Marekani na China ulimtangulia Trump,umekuwa mkali zaidi na wenye kueleweka zaidi.
Hatari za diplomasia ya Twitter
Kuhusiana na mawasiliano ya sera ya kigeni, Trump na utawala wake wametoa ujumbe mchanganyiko kwa nyakati tofauti na kupitia njia tofauti za mawasiliano - mojawapo ni akaunti binafasi ya Trump ya mtandao wa Twitter, ambao mara nyingi inakuwa na maneo makali.
Alexei Drew, anaetafiti kuhusu mitandao ya kijamii na kuongezeka kwa mizozo katika taasisi ya sayansi na masuala la usalama ya chuo cha King's College mjini London, anazungumzia uhusiano wa Marekani na Iran kama mfano halisi wa namna diplomasia ya Twitter ya Trump ilivyoyafanya makabiliano ya kimataifa kuwa magumu na hatari zaidi.
Soma pia: Marekani yatakiwa kutafakari upya uamuzi wake kuhusu WHO
"Ni vigumu sana, ukijiweka katika nafasi ya (waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Javad Mohammed) Zarif na Wairan, kubani ni upi hasa msimamo wa Marekani wakati ukiwa ni taarifa mkanganyiko zinazotoka mara kwa mara wizara ya mambo ya nje na maelezo yanayotofautiana ya Donald Trump," Drew alisema. "Kuna wizara ya ulinzi, kuna maelezo yote hayo. Hawaoanishi ujumbe wao na maudhui zao."
Drew haamini iwapo Twitter pekee yake inaaeza kuanzisha mzozo. Hata hivyo, "Matumizi ya Twitter katika mfumo uliopo wa uchochezi au mazingira au mzozo wa kihistoria kati ya watendaji wa serikali au vinginevyo yanaweza kuepelekea yasiyokusudiwa au kuongezeka zaidi ya kile ambacho kingetokea iwapo Twitter isingetumiwa."
Amewaimarisha watawala wa kiimla
Athari zaidi ya miaka minne ya Donald Trump ni kwamba watawala wa kiimla wamejiimarisha zaidi kwenye jukwaa la kimataifa. Wakati wengi walikuwa madarakani kabla ya Trump, namna anavyohusiana nao, kuanzia mambo yasiyo muhimu hadi kuwahusudu, inatilia mkazo uidhinishaji wake wa mfumo wao wa utawala na kufichua hali ya kutokuwa tayari kuzungumzia madai ya ukiukaji.
Soma pia: Trump ammwagia sifa Modi ziarani India
Mfano mmoja ni msimamo wa Trump kuelekea Saudi Arabia baada ya mauaji ya Jamal Khashoggi. Katikati wa ushahidi unaoongezeka kwamba wanachama wa ngazi ya juu wa familia ya kifalme ya Saudi Arabia walihusika katika kifo cha mwanahabari huyo, Trump aliezea kuiunga mkono serikali ya Saudi Arabia.
Chini ya Trump, "Viongozi wa kiimla hawatapata upinzani wowote kutok Marekani kwa sasa," MacMillan alisema.
Chanzo: DW