Ni upi urathi wa sera ya kigeni ya Merkel?
6 Septemba 2021Ni wachache sana nje ya Ujerumani waliomfahamu Angela Merkel wakati alipochaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa kansela mwaka 2005.
Na ni wachache pia walifikiria ni kwa kiwango gani angeshawishi siasa za ulimwengu.
Alianza haraka kujiamini, kote nyumbani na nje. Kuanzia mwanzo, aliunda kwa sehemu kubwa mkakati wa sera ya kigeni wa serikali yake mwenyewe, kuliko kumuachia jukumu hilo waziri wa mambo ya kigeni.
Soma pia: Warithi watarajiwa wa Merkel watofautiana kuhusu China, Urusi
Kama mwenyeji wa mkutano wa kilele wa viongozi wa mataifa manane yalioendelea kiviwanda G8, uliofanyika katika eneo la mapumziko la pwani ya Baltic la Heiligendamm mwaka 2007, alikuwa tayari anashughulikia kwa kujiamini, wakuu muhimu zaidi wa mataifa na serikali duniani.
Ukitazama nyuma, inaonekana kama dunia nyepesi isiyo na changamoto zozote.
Ujerumani yachukua uongozi mzozo wa sarafu ya Euro
Hata hivyo, kansela huyo aliingia kwenye kushughulikia mizozo: Mwaka 2008 ulitokea mzozo wa kifedha wa dunia.
Sarafu ya Euro, ambayo ni moja ya viashiria imara zaidi vya muungano wa Ulaya, ilikabiliwa na shinikizo, na kupelekea moja ya kauli maarufu za Merkel alipoonya kwamba "Euro ikifeli, basi Ulaya inafeli."
Soma pia: Je, kiongozi wa chama cha Kijani Annalena Baerbock anaweza kuwa kansela ajae wa Ujerumani?
Chini ya Merkel, taifa lake lenye uchumi imara zaidi katika kanda ya Umoja wa Ulaya lilijitwika jukumu la uongozi barani Ulaya.
Kwa upande mmoja, serikali ya Ujerumani ililaazimisha hatua kali za kubana matumizi na mageuzi hasa kwa mataifa yenye mzigo mkubwa wa madeni: Nchini Ugiriki, baadhi ya wakosoaji walitoa hata ulinganisho na ukaliaji wa Ujerumani wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Kwa upande mwingine, Merkel aliidhinisha msaada mkubwa kwa mataifa ya Ulaya. Dhamana ya Ujerumani kwa madeni ya mataifa mengine iliongezeka pakubwa.
Ukweli kwamba sehemu iliyobaki ya Umoja wa Ulaya, kwa ujumla ulikubali jukumu jipya la uongozi wa Ujerumani pia ulitokana na haiba ya Merkel.
Anachanganya utamaduni wa kujizuwia na utamaduni wa uwajibikaji, kama alivyoliweka mtaalamu wa siasa Johannes Varwick kutoka Chuo Kikuu cha Halle, katika mahojiano na DW.
Ufaransa na Ujerumani: Majirani na washirika wasio karibu sana
Jukumu linaloongezeka la Ujerumani pia lilisababisha ukosefu wa urari wa madaraka na Ufanara.
Merkel alikuwa amejifunga kikamilifu kwa mshirika huyu wa karibu, kiasi kwamba vyombo vya habari vikabuni jina la Merkozy kutokana na uhusiano wake mzuri na rais wa wakati huo wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy.
Lakini aliacha matakwa ya marais mbalimbali wa Ufaransa, ikiwemo la karibuni zaidi la Emmanuel Macron, la kuuimarisha zaidi Umoja wa Ulaya, kwa mfano kwa kuunda nafasi ya waziri wa fedha wa kanda ya euro, kufifia.
Hiyo ilikuwa fursa iliyopotea, kwa mujibu wa Henning Hoff kutoka Baraza la uhusiano wa nje la Ujerumani.
Na kumekuwepo na kutengwa kunakoongezeka kutoka Ufaransa kwa mujibu wa mtaalamu wa siasa Varwick, na kuongeza kwamba Merkel hakuwa na maono makubwa kuhusiana na kuuimarisha Umoja wa Ulaya.
Avutiwa na China
Mbali na hilo, kansela Merkel aliendeleza sera ya kigeni ya serikali zilizotangulia, ya kutoegemea upande, inayozingatia biashara, na kukubaliana na pande zote pale inapowezekana -- wakati ikiwa na jicho kwenye maslahi ya kiuchumi ya Ujerumani kote duniani.
Soma pia:Maoni: Mkutano wa kilele kati ya Ulaya na China wakosa tija
Mkakati huu ulishuhudia biashara hasa na China ikikua haraka. Merkel alisafiri mara kwa mara kwenda China na alionekana kufurahishwa.
Hoff aliona uvutiwaji wake na nguvu ya kiuchumi ya China ikikaribia heshima ya uoga. Masuala ya haki za binadamu yalikuwa yakiibuliwa naye tu kwa tahadhari akiwa huko.
Sera ya ukarimu ya wakimbizi
Hakuna kilichompa umaarufu zaidi duniani Merkel -- na hakuna kilichougawa umma kumhusu ndani na kimataifa, kuliko uamuzi wake wa kuiacha wazi mipaka ya Ujerumani kwa ajili ya maelfu ya wakimbizi na wahamiaji walioingia nchini humo Agosti na Septemba 2015.
Soma piaMerkel ataka operesheni ya kuokoa wahamiaji ianze tena
Alitetea uamuzi huo kwa uhisani wa Kikristo, na vile vile uzoefu wake kama raia wa Ujerumani ya Ukomunisti ya Magharibi - GDR, na mipaka yake isiyopenyezeka.
Merkel alipiga picha na wakimbizi wa Syria, na Ujerumani ikageuka sehemu ambayo watu kutoka kote duniani waliiangalia kwa matumaini ya maisha bora.
Alichaguliwa kuwa "Mtu wa Mwaka" na jarida la Time, lililomtaja kuwa Kansela wa Dunia Huru."
Wengine, hasa serikali za mataifa wanachama wa EU ya Ulaya Mashariki, yalimchukia kwa kujaribu kulazimisha sera yake ya ukarimu ya hifadhi kwa kanda nzima ya Umoja wa Ulaya.
Tangu wakati huo, siasa kali za mrengi wa kulia zimeshamiri barani Ulaya.