1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUfaransa

Ufaransa kutoa mafunzo ya kutumia ndege za kivita za Mirage

8 Juni 2024

Rais Emmanuel Macron amesema Ufaransa inapanga kuanza mara moja kuwafunza marubani na mafundi wa Ukraine namna ya kuziendesha ndege za kivita aina ya Mirage, ambazo imeahidi kuzipeleka Kyiv.

https://p.dw.com/p/4goBv
Maadhimisho ya D Day nchini Ufaransa. Macron na Zelensky
Rais Emmaneu Macron wa Ufaransa na Volodymyr Zelensky wa Ukraine wakiteta jambo wakati walipokutana nchini UfaransaPicha: Ludovic Marin/Pool via REUTERS

Amesema hayo baada ya mazungumzo na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika makazi ya rais ya Élysée jijini Paris.

Macron hata hivyo bado hajaainisha idadi ya ndege ambazo Ufaransa na mataifa mengine wanataraji kuzipeleka Ukraine ambayo inapambana na Urusi.

Ufaransa bado inahitaji kuhitimisha mchakato huo kwa kuamua juu ya idadi ya ndege itakayopeleka pamoja na mazungumzo ya mpango wa pamoja ulioanza miezi kadhaa iliyopita na mataifa washirika.