UchumiUganda
Uganda yasaini mkataba wa ujenzi wa reli ya SGR na Uturuki
16 Oktoba 2024Matangazo
Waziri wa Uchukuzi wa Uganda Katumba Wamala amesema hapo jana kuwa mradi huo wa kilometa 272 za reli ya mwendo kasi inayotumia umeme (SGR), utaanza mwezi Novemba na kutokea katika mji mkuu wa Uganda Kampala hadi Malaba kwenye mpaka na Kenya na utakamilika baada ya miaka minne.
Waziri Wamala amesema mradi huo unalenga kuondokana na ucheleweshaji wa muda mrefu wa kusafirisha bidhaa kutoka bandari ya Mombasa ambayo ndio lango kuu la biashara ya Uganda.
Treni hizo zitasafiri kwa kasi ya kilomita 120 kwa saa na mradi huo utakuwa na uwezo wa kubeba tani milioni 25 kwa mwaka.