Uingereza kuanza kuwapeleka wahamiaji Rwanda Julai Mosi
4 Mei 2024Matangazo
Jaji Martin Chamberlain alifichua tarehe hizo alipokuwa akipanga kusikilizwa kwa pingamizi lijalo la kisheria kwa sheria hiyo mpya ya uhamiaji.
Pingamizi hilo liliwasilishwa na chama cha wafanyakazi wa umma nchini humo. Sheria mpya ya uhamiaji nchini Uingereza inaruhusu mawaziri kupuuza sehemu za sheria za ndani na za kimataifa wakati wa kuamua juu ya uhamishaji huo wa lazima kwa waomba hifadhi.Aprili 22, Waziri Mkuu Rishi Sunak alisema kwamba alitarajia safari za kwanza za ndege kuondoka ndani ya "wiki 10 hadi 12", lakini hakutoa tarehe kamili.