Ujerumani hatarini kupoteza sifa ya utengenezaji magari
4 Septemba 2023Matangazo
Hayo yameelezwa na rais wa chama cha sekta ya utengenezaji magari cha Ujerumani VDA,Hildegar Müller ambaye amesisitiza kwamba japokuwa makampuni ya utengenezaji magari nchini Ujerumani watanusurika,nchi hiyo haitoweza kubakia na sifa yake kama kitovu cha utengenezaji magari,bila ya kufanyika mageuzi makubwa.
Soma pia:Teknolojia ya Akili bandia huenda ikasababisha ubaguzi
Müller ametowa mtazamo huo kabla ya maonesho makubwa ya biashara ya magari IAA yanayofanyika mjini Munich.
Miongoni mwa sababu kubwa alizozitaja kuchangia matatizo,ni kuwepo kwa kasi ndogo ya maamuzi ya kisiasana mpango wa kisheria kwaajili ya kusimamia masuala kama teknolojia ya akili bandia.