1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuipa Ukraine msaada wa kijeshi euro bilioni 2.7

13 Mei 2023

Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani imesema leo kuwa inajiandaa kupeleka msaada mpya wa vifaa vya kijeshi nchini Ukraine vyenye thamani ya euro bilioni 2.7

https://p.dw.com/p/4RIeQ
Deutschland Bundeswehr Leopard 2 Panzer
Picha: Alexander Koerner/Getty Images

Msaada huo unaoelezwa kuwa mkubwa kabisa kuwahi kutolewa na Ujerumani, tangu Urusi ilipoivamia Ukraine.

Msaada huo utajumuisha magari 20 ya kivita chapa ya Marder, vifaru 30 chapa Leopard 1,vifaru 15 chapa Gepard kwa ajili ya mfumo wa ulinzi wa anga, ndege 200 zisizo na rubani na zaidi ya magari 200 yatakayotumika kijeshi na kwa ajili ya usambazaji wa vifaa. 

Wakati huo huo, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema leo kuwa vikosi vya Urusi vimeondoka katika mji wa Bakhmut siku nne zilizopita.

Katika taarifa yake ya kijasusi ya kila siku, Uingereza imesema kuondoka kwa vikosi vya Urusi kumevifanya vikosi vya Ukraine kurejesha takribani kilomita moja ya eneo hilo.