Sheria na HakiAfrika
Ujerumani na Somalia kuwafukuza wahamiaji haramu
6 Novemba 2024Matangazo
Baada ya mkutano na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud mjini Berlin, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema viongozi hao walikubaliana kuwa wahamiaji wasiokuwa na haki ya kisheria kusalia Ujerumani "watarudishwa makwao haraka na kwa ufanisi."
Scholz amesema watakaoathirika zaidi na hatua hiyo ya kufukuzwa ni wahalifu wa makosa makubwa.
Soma pia:Polisi ya Ujerumani yasema idadi ya wanaovuka mpaka yapungua
Kansela huyo ameongeza kuwa uamuzi huo pia ni wa kuyalinda maslahi ya jamii kubwa kabisa ya Wasomali wanoishi Ujerumani na ambao wanaendelea vizuri na wametangamana katika jamii.
Jumla ya Wasomalia 65,000 wanaishi Ujerumani. Kansela Scholz amesema ni idadi ndogo pekee ambao hawana haki ya kuishi nchini humo.