Ujerumani yakabiliwa na mzozo wa bajeti
4 Desemba 2023Matangazo
Mgogoro wa bajeti umetokana na uamuzi uliotolewa na mahakama ya katiba ambao umesababisha nakisi ya Euro bilioni 60 katika mipango ya matumizi ya serikali.
Msemaji wa wizara ya uchumi ameeleza kuwa uwepo wa makamu wa kansela huyo mjini Berlin ni jambo la lazima ili kuyasogeza mbele majadiliano juu ya bajeti ya mwaka ujao.
Soma zaidi: Je, kiongozi wa chama cha Kijani Annalena Baerbock anaweza kuwa kansela ajae wa Ujerumani?
Habeck, ambaye pia ni waziri wa uchumi na mazingira. alikuwa ashiriki hapo kesho kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya tabia nchi unaoendelea mjini Dubai (COP28).
Waziri huyo amesema anaona pana hatua zinazopigwa katika mazungumzo juu ya bajeti inayopaswa kupitishwa mnamo mwezi huu.