Ujerumani yaunga mkono Nigeria kuwa kwenye G20
31 Oktoba 2023Matangazo
Akizungumza akiwa ziarani Lagos, Scholz amesema ukweli kwamba nchi kubwa kama Nigeria, ambayo ndiyo kubwa zaidi kiuchumi barani Afrika, inadai kuwa sehemu ya kundi hilo, ni sahihi.
Kansela huyo wa Ujerumani ameongeza kuwa kukubaliwa kwa Umoja wa Afrika - AU katika kundi hilo kunaashiria mafanikio, lakini hiyo haitoshi.
Soma zaidi: Ujerumani kufanya biashara ya nishati na Nigeria
Aidha, alibainisha kuwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halina wawakilishi wa kudumu kutoka Afrika au Amerika Kusini.
Ujerumani kwa muda mrefu imekuwa ikishinikiza mageuzi ya chombo muhimu cha Umoja wa Mataifa.
Awali, Scholz aliielezea Nigeria kuwa mshirika muhimu kwa Ujerumanikatika uzalishaji wa gesi ya haidrojeni na kisha ununuzi wa gesi asilia.