Ujerumani kufanya mazungumzo na mamlaka mpya ya Syria
17 Desemba 2024Matangazo
Ikiungana na Marekani pamoja na Uingereza katika harakati za kuwa na mawasiliano na kundi hilo baada ya kuuangusha utawala wa Bashar Al Assad. Msemaji wa serikali ya Ujerumani amesema mazungumzo ya Ujerumani na wawakilishi wa kundi hilo yatazingatia kipindi cha mpito kwa Syria na ulinzi wa makundi ya wachache. Mgogoro wa Syria ulioanza mwaka 2011 ulisababisha wakimbizi zaidi ya milioni moja kukimbilia Ujerumani. Na kuanguka kwa Utawala wa Assad kumezua gumzo nchini Ujerumani kuhusu mchakato wa waomba hifadhi kutoka Syria uliositishwa kwa sasa ili kufuatilia hali nchini humo.