1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yawasilisha mswada wa kuharakisha uhamishaji

8 Septemba 2024

Serikali ya Ujerumani imewasilisha pendekezo la mikakati ya kuharakisha uhamishaji wa wahalifu na kupunguza uhalifu wa kutumia visu.

https://p.dw.com/p/4kP5b
Rais wa Syria, mshukiwa wa uhalifu wa kutumia kisu Solingen asindikizwa na polisi kuelekea ofisi ya mwendesha mashtaka huko Karlsruhe, Ujerumani mnamo Agosti 25,2024
Rais wa Syria, mshukiwa wa uhalifu wa kutumia kisu Solingen asindikizwa na polisi kuelekea ofisi ya mwendesha mashtaka huko Karlsruhe, UjerumaniPicha: Heiko Becker/REUTERS

Waziri wa Mambo ya Ndani, Nancy Faeser, ameliambia shirika la habari la dpa mjini Berlin kwamba wanatoa ulinzi zaidi dhidi ya ugaidi wa itikadi kali, uhamishaji wa wahalifu, marufuku ya visu na kutambulishwa kwa wahalifu.

Soma pia:Ujerumani kuongeza kasi ya kuwarudisha wahamiaji makwao

Awali, Waziri wa Sheria Marco Buschmann, alisema kuwa muungano wa vyama vitatu wa Kansela Olaf Scholz, ulikubaliana juu ya maelezo ya pendekezo hilo linalolenga kuimarisha usalama kufuatia shambulizi hilo la Solingen, ambalo watu watatu waliuawa na rai mmoja raia wa Syria mwenye umri wa miaka 26.

Vyama vya muungano na upinzani kukutana Jumanne 

Vyama hivyo vitatu vya muungano pamoja na upinzani wa kihafidhina vinatarajiwa kukutana Jumanne na viongozi wa majimbo 16 nchini humo kujadili msimamo wa pamoja.