Wajumbe wa vyama wakutana kujadili mashambulio ya Solingen
3 Septemba 2024Hii ni baada ya mkasa katika mji wa Solingen ambapo watu walichomwa visu kwenye tamasha lililofanyika kwenye mji huo uliopo katika jimbo la magharibi mwa Ujerumani.
Wajumbe kwenye mkutano huo watazingatia mpango wa usalama uliotangazwa na serikali ya Kansela Olaf Scholz wiki iliyopita kwa lengo la kutoa jibu la shambulio la Solingen ambapo watu watatu waliuliwa na wengine wanane walijeruhiwa.
Soma pia: Watu 6 wajeruhiwa katika shambulio jipya la kisu Ujerumani
Mtuhumiwa ni mtu anayedaiwa kuwa mwenye itikadi kali kutoka Syria.
Amewekwa kuzuizini kwa kosa la mauji. Wanaohudhuria mkutano huo wa mjini Berlin ni pamoja na waziri wa mambo ya ndani Nancy Faeser, atakaeongoza mkutano huo, waziri wa sheria Marco Buschmann na waziri mambo ya nje Annalena Baerbock.