Ukraine kupokea bilioni dola 1.5 kusaidia kujijenga upya
30 Juni 2023Matangazo
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Telegram, Waziri Shmyhal amesema fedha hizo zitatolewa kwa dhamana ya serikali ya Japan na zitasaidia kuboresha mifumo ya kijamii na maendeleo ya kiuchumi.
Ukraine inategemea msaada wa kifedha kutoka kwa washirika wake wa kigeni ili kuweza kufidia nakisi ya bajeti yake. Jana, bodi ya Shirika la Fedha la Kimataifa ilikamilisha mkakati wa mkopo na hivyo kuiruhusu Kyiv kupewa mara moja dola milioni 890 ili kusaidia bajeti yake.
Ukraine inaendelea na ujenzi upya wa shule, hospitali, barabara na madaraja na kufanya ukarabati katika sekta ya nishati licha ya kuendelea mapigano kusini na mashariki mwa nchi hiyo.