1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yadaiwa kuwapeleleza askari wa Ukraine walio mafunzoni

Zainab Aziz Mhariri: Mohammed Khelef
26 Agosti 2022

Nguvu za umeme kwenye gridi ya taifa ya umeme nchini Ukraine baada ya kukatika kutoka kwenye kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia. Na Urusi yadaiwa kuwapeleleza askari wa Ukraine wanaopata mafunzo nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4G6ER
Deutschland | Training von Soldaten aus der Ukraine
Picha: U.S. Army/ZUMA Press/picture alliance

Shirika linalosimamia umeme nchini Ukraine - Energoatom, limetoa taarifa kwamba kinu hicho cha Zaporizhzhia kituo kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya kilikatwa kutoka kwenye mtandao wa umeme wa nchini Ukraine kwa mara ya kwanza katika historia yake hapo jana siku ya Alhamisi lakini hadi kufikia saa nane usiku wa kuamkia leo mtambo huo uliunganishwa tena kwenye gridi ya taifa nakuanza kutoa umeme kwa ajili ya mahitaji ya watu wa Ukraine.

Wakati huo huo mkurugenzi wa shirika la kimataifa la kudhibti nishati (IAEA ) bwana Rafael Grossi amesema yuko tayari kuzuru Zaporizhzhya na kundi la wataalam. Lakini, hata hivyo hakuna makubaliano yaliyofikiwa kuhusu jinsi ya kuwapeleka watalaamu hao kwenye eneo hilo.

Mkurugenzi wa shirika la kimataifa la kudhibti nishati (IAEA ) Rafael mariano Grossi.
Mkurugenzi wa shirika la kimataifa la kudhibti nishati (IAEA ) Rafael Mariano Grossi.Picha: Askin Kiyagan/AA/picture alliance

Mkurugenzi wa shirika la kimataifa la kudhibti nishati (IAEA ) Rafael Grossi amesema mapigano karibu na kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia yamezusha hofu ya kutokea maafa ya mionzi ya nyuklia inaoweza kuathiri eneo la karibu na kinu hicho na maeneo mengine mengi katika bara la Ulaya, kama vile ajali ya kinu cha nyuklia cha Chernobyl ya mwaka 1986.

Hapa nchini Ujerumani kikosi cha jeshi cha kukabiliana na ujasusi nchini Ujerumani (MAD) kimeeleza kwamba kuna dalili Urusi iliwapeleleza Waukraine wanaofanya mafunzo nchini Ujerumani,hayo ni kwa mujibu wa gazeti la Der Spiegel ambalo limripoti leo Ijumaa. Tangu kuanza kwa mafunzo katika maeneo mawili ya kijeshi, jeshi la Ujerumani la kukabiliana na ujasusi limesema limegundua magari yanayotiliwa shaka ambayo yana uwezo wa kuona umbali wa kutoka kwenye barabara za kuingia kwenye kambi hizo mbili za kijeshi.

Kulia Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz. Kushoto: Jenerali ya jeshi la Ujerumani, Carsten Breuer.
Kulia Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz. Kushoto: Jenerali ya jeshi la Ujerumani, Carsten Breuer. Picha: Steffen Kugler/Bundespresseamt/dpa/picture alliance

Waukraine wanafanya mazoezi katika kambi za Idar-Oberstein katika jimbo la  Rhineland-Palatinate na Grafenwöhr katika jimbo la Bavaria. Urusi inadaiwa kuyapeleleza maeneo yote hayo mawili. Jeshi la Ujerumani linawafunza wanajeshi wa Ukraine juu ya matumizi ya silaha ya howitzer 2000 na vikosi vya Marekani vinatoa mafunzo kwa Waukraine juu ya mifumo ya silaha za Magharibi.

Vyanzo:/AFP/DPA/AP/https://p.dw.com/p/4G4VF