1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Miundombinu ya nishati ya Ukraine yashambuliwa na Urusi

30 Machi 2024

Ukraine imetangaza hatua ya mgao wa umeme katika baadhi ya mikoa baada ya Urusi kuishambulia vikali miundombinu yake ya nishati.

https://p.dw.com/p/4eGVJ
Ukraine- Mkoa wa Kherson
Miundombinu ya nishati katika Kijiji cha Oleksandrivka katika mkoa wa Kherson nchini UkrainePicha: Igor Burdyga/DW

Mikoa iliyoathirika zaidi na hatua hiyo ni Dnipropetrovsk, Zaporizhzhia, Kirovograd, Kharkiv na Kryvyi Rih.

Katika ombi jipya kwa washirika wa Magharibi, Waziri Mkuu wa Ukraine Denys Shmygal amesema Ukraine inahitaji mifumo zaidi ya ulinzi wa anga huku Ikulu ya White House ikilitaka Bunge la Marekani kupitisha mswada wa kufadhili ulinzi wa Ukraine.

Soma pia: Ukraine yasema mashambulizi yanahatarisha ugavi wa umeme

Kwa upande wake Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema ikiwa nchi yake haitopata msaada uliozuiwa na Bunge la Marekani, vikosi vyake vitalazimika kurudi nyuma katika uwanja wa vita, jambo ambalo amesema litainufaisha Urusi ambayo inaweza kuchukua udhibiti wa miji mikubwa.