Ukraine yakanusha kusambaza droni kwa waasi nchini Mali
15 Oktoba 2024Gazeti la Ufaransa Le Monde liliripoti kuwa wapiganaji wa kundi la Tuareg nchini Mali wanatumia droni za Ukraine kwa usaidizi wa kisiri wa Ukraine dhidi ya jeshi la Mali na kundi la mamluki wa Urusi la Wagner.
Ukraine yapinga kujihusisha na waasi wa Tuareg nchini Mali
Katika taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Ukraine, imesema nchi hiyo inapinga vikali shtuma hizo ambazo zimeripotiwa na vyombo vya habari vya kimataifa kuhusu madai ya kuhusika kwake katika usambazaji wa droni kwa waasi nchini Mali.
Mali, ambapo maafisa wa kijeshi walinyakua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 2020 na 2021, inapambana na uasi wa makundi ya itikadi kali wa miaka mingi, huku mapigano makali dhidi ya waasi wa Tuareg yakiendelea karibu na mpaka kati ya nchi hiyo na Algeria.