1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Ukraine yasitisha mkataba wa usafirishaji wa gesi ya Urusi

2 Januari 2025

Ukraine imesema usafirishaji wa gesi ya Urusi kupitia nchi hiyo kwenda Ulaya umesitishwa kama ulivyopangwa.

https://p.dw.com/p/4okkM
Russia | Gazprom | Ukraine
Bomba la kusafirisha gesi ya UrusiPicha: EPA/Maxim Shipenkov/dpa/picture alliance

Ukraine imesema kwa sasa kampuni ya usafirishaji wa gesi ya Urusi ya Gazprom haina njia yoyote ya halali au kiufundi kupeleka gesi kupitia taifa hio, baada ya Kiev kuridhia mkataba wa miaka mitano kati ya kampuni ya usafirishaji wa gesi ya Ukraine, Naftogaz, na ile ya Urusi, Gazprom, kukamilika.

Soma pia: Umoja wa Ulaya kutumia njia mbadala kuagiza gesi

Rais wa Ukraine  Volodymyr Zelensky amesema hapo jana kwamba hatua hiyo ni pigo na ishara ya kushindwa kwa Moscow katika vita vyake na Ukraine.

Kufungwa kwa mabomba hayo ya kusafirisha gesi kulitarajiwa kutokana na uvamizi wa Urusi Ukraine mnamo Februari 2022 huku Ukraine ikiweka wazi kwamba haitaurefusha mkataba huo.