Ulaya yaipa Uturuki bilioni 1 kuwasaidia wakimbizi wa Syria
17 Desemba 2024Matangazo
Von der Leyen amesema ufadhili huo mpya unaongeza kiwango cha fedha cha bilioni 10 ambacho Uturuki imepokea tangu mwaka 2011, kuwasaidia watu waliokuwa wakikimbia mateso ya utawala wa Bashar al-Assad, ambao sasa umeangushwa. Fedha hizo pia zitasaidia katika masuala ya elimu na huduma za afya kwa wakimbizi hao: Uturuki na mataifa ya Umoja wa Ulaya yametoa hifadhi kwa wakimbizi wa Syria, lakini Ankara inasemekana kuwa na idadi kubwa zaidi ya wakimbizi hao nchini mwake wakifikia milioni 3 huku zaidi ya milioni moja wakipewa ulinzi wa kimataifa Ulaya.