1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa walaani mauwaji ya raia Gaza

11 Mei 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani kuuwawa kwa raia katika eneo la Gaza kwa kusema ni kitendo kisichokubalika na kuzitaka pande hasimu katika eneo hilo kujizuia haraka na vurugu.

https://p.dw.com/p/4RBAj
Israel Palästina Nahost-Konflikt
Picha: SAID KHATIB/AFP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani kuuwawa kwa raia katika eneo la Gaza kwa kusema ni kitendo kisichokubalika na kuzitaka pande hasimu katika eneo hilo kujizuia haraka na vurugu.

Jeshi la Israel kwa siku mbili mfululizo liliyalenga maeneo wa wanamgambo wa Kipalestina huko Gaza huku wanamgambo hao wakivurumisha mamia ya roketi hadi Tel Aviv,katika kipindi ambacho  Misri ikianzisha juhudi za kupatanisha, kukomesha mapigano hayo.

Soma zaidi:Israel na wanamgambo wa Kipalestina warushiana makombora Gaza

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 15 lilikutana kwa mkutano wake wa ndani Jumatano kutokana na vurugu hizo. Kwa jumla Wapalestina 20, wakiwemo wanawake watano na watoto watano, pamoja na makamanda watatu waandamizi wa wanamgambo hao na watu wanne wenye kujihami kwa silaha wameuawa tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi hayo Jumanne iliyopita.