1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiHaiti

UN: Kutumike nguvu kupambana na magenge ya uhalifu Haiti

16 Agosti 2023

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitolea mwito jamii ya kimataifa kupeleka kikosi maalumu cha kimataifa kitakachojumuisha wanajeshi na polisi nchini Haiti kukabiliana na magenge ya uhalifu yenye silaha za kisasa.

https://p.dw.com/p/4VE3g
Hali mbaya ya usalama Haiti
Maafisa wa polisi Haiti wakipiga doria katika mji wa Port-au-PrincePicha: Rodrigo Abd/AP Photo/picture alliance

Taarifa hii ni kulingana na ripoti ya Antonio Guterres kwa Baraza la Usalama la Umoja huo, iliyoonekana na shirika la habari la Reuters jana Jumanne.

Ripoti ya Guterres iliyosambazwa kwa wanachama wote 15 wa baraza hilo jana, ilitaja machaguo mawili makubwa, ambayo ni msaada wa vifaa kwa vikosi vya kimataifa na polisi ya Haiti pamoja na kuimarisha ujumbe wake uliopo nchini humo.

Haiti iliomba msaada wa kimataifa mwaka uliopita wa kupambana na magenge ya kihalifu yaliyouelemea mji mkuu Part- au- Prince.