1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yathibitisha kuwa jeshi la Rwanda linashirikiana na M23

8 Julai 2024

Takriban wanajeshi 3,000 hadi 4,000 wa Rwanda wanapambana na jeshi la Kongo wakishirikiana na waasi wa M23 katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4i0oy
DR Kongo
Baadhi ya waasi wa M23 Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Hayo ni kulingana na ripoti ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa ambayo shirika la habari la AFP limepata nakala yake leo Jumatatu.

M23 yaendelea kuchukua udhibiti wa maeneo mashariki mwa Kongo

Ripoti kutoka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ilibainisha kuwa jeshi la Rwanda "lina udhibiti na hutoa mwelekeo wa operesheni za M23", jambo linazozifanya mamlaka za Rwanda kubebeshwa dhima kwa vitendo vya M23. Serikali mjini Kigali imekuwa ikikanusha vikali shutuma hizo.