UN yatoa dola milioni 100 kukabiliana na matukio ya dharura
31 Agosti 2024Matangazo
Joyce Msuya, Kaimu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu amesema mataifa hayo yanakabiliwa na ukosefu wa fedha na hivyo kupelekea mashirika ya kibinaadamu kushindwa kutoa msaada muhimu wa kuokoa maisha ya watu.
Zaidi ya theluthi moja ya ufadhili huo mpya utatolewa kwa Yemen inayokumbwa kwa miaka 10 sasa na vita vya wenyewe kwa wenyewe pamoja na Ethiopia inayokabiliana na makundi ya uasi. Mataifa mengine yatakayopokea msaada huo ni pamoja na Myanmar, Mali, Burkina Faso, Haiti, Cameroon, Msumbiji, Malawi na Burundi.