UchumiMisri
Umoja wa Ulaya kuipa Misri ufadhili wa euro bilioni 7.4
17 Machi 2024Matangazo
Hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa kushinikiza kuzuia mtiririko wa wahamiaji wanaopitia katika Bahari ya Mediterania kuingia ulaya. Umoja wa Ulaya umetangaza hivi punde kuidhinisha msaada wa euro bilioni 7.4 kwa Misri.
Kwa muda mrefu, serikali za nchi za Magharibi zimekuwa na wasiwasi kuhusu hali ya sintofahamu katika nchi ya Misri yenye watu milioni 106, ambayo imekuwa ikikabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi na hivyo kupelekea idadi inayoongezeka ya watu kuihama nchi hiyo.
Mpango huo ambao umekosolewa na mashirika ya kutetea haki za binaadamu, unalenga kuimarisha ushirikiano katika sekta za nishati mbadala, biashara na usalama. Fedha hizo zitatolewa kama misaada, mikopo na ufadhili mwingine katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.