1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Mafuriko Somalia yasababisha uharibifu mkubwa

16 Mei 2023

Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa amesema mafuriko yaliyosababishwa na mvua za msimu Somalia, yamesababisha uharibifu huku nyumba za makazi na mashamba vikisombwa na maji na vituo vya afya vikilazimika kufungwa.

https://p.dw.com/p/4RSFB
Äthiopien | Überflutung in Konso-Zone
Picha: Shewangizaw Wegayehu/DW

Stephane Dujarric amesema kulingana na makadirio ya awali, watu wasiopungua watano wamekufa na zaidi ya wengine 460,000 wameathiriwa na mafuriko hayo.

Watu wapatao 219,000 wakiwemo pia wanawake na watoto wamelazimika kuyahama makazi yao.

Uharibifu mkubwa umeshuhudiwa katika jimbo la kati la Hiiraan huko Hirshabelle ambapo maelfu ya watu wamehamishiwa huko Beledweyne.

Dujarric amesema ikiwa mvua zitaendelea nchini Somalia, wanakadiria kuwa hadi watu milioni 1,6 wanaweza kuathiriwa na mafuriko.