1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Watu 184 wafariki dunia Haiti kutokana na ghasia

9 Desemba 2024

Mkuu wa kitengo cha haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Kamishna, Volker Turk, amesema watu 184 wameuawa katika mji mkuu wa Haiti kutokana na ongezeko la ghasia za magenge.

https://p.dw.com/p/4nvkg
Haiti, Port-au-Prince | Streitkräfte patrouillieren in Vorort Pétion-Ville nach Bandenangriff
Picha: Clarens Siffroy/AFP/Getty Images

Amesema watu hao wapatao 184 waliuawa mwishoni mwa wiki iliyopita katika mji mkuu huo Port-au-Prince.

Kamishna Turk aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba mauaji hayo yanafanya idadi ya vifo mnamo mwaka huu pekee nchini Haiti ifikie watu 5,000. 

Ukosefu wa usalama nchini Haiti, ambao tayari ni mbaya baada ya miongo kadhaa ya ukosefu wa utulivu wa kisiasa, uliongezeka zaidi mapema mwaka huu wakati makundi yenye silaha yalipoanzisha mashambulizi katika mji mkuu.

Magenge hayo yalilenga shabaha ya kumpindua waziri mkuu wa wakati huo, Ariel Henry.

Magenge hayo bado yanadhibiti asilimia 80 ya mji mkuu licha ya uwepo wa polisi wa Kenya wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa pamoja na Marekani.