UN yamteua Sigrid Kaag kama mratibu mpya wa misaada Gaza
27 Desemba 2023Matangazo
Tangazo hilo lililotolea na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres limekuja baada ya Baraza la Usalama la umoja huo, kupitisha azimio lililompa nafasi ya kumteua mratibu maalum kwaajili ya Gaza ambako zaidi ya watu milioni 2 wanauhitaji mkubwa wa dharura wa maji, chakula na dawa. Kaag anatarajiwa kuanza kuratibu majukumu yake Tarehe 8 Januari
Soma pia:Hamas yakataa pendekezo la kusitisha mapigano kwa muda
Watu zaidi ya 20,000 wakiwemo watoto 8000 wameuwawa tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamasmnamo Oktoba 7. Marekani, Umoja wa Ulaya na nchi kadhaa za Magharibi zimeliorodhesha kundi la Hamas kama kundi la kigaidi.