UN yatoa wito kwa Israel na Hezbollah kusitisha mvutano
21 Septemba 2024Bi Rosemary ametahadharisha kuwa iwapo vita kamili vitatokea kati ya Israel na Hezbollah huenda vikasababisha uharibifu mkubwa zaidi kuliko ule ulioshuhudiwa hadi sasa.
Ametoa rai hiyo kwa wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa baada ya kulipuka kwa vifaa vya mawasiliano vya Hezbollah ambapo watu 37 waliuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa.
Soma pia: Hizbullah, Israel washambuliana vikali
Waziri wa mambo ya nje wa Lebanon Abdallah Bou Habib ameilaumu Israel kwa kuhusika na hujuma hiyo na kuongeza kuwa hakuna mtu yoyote duniani aliye salama.
Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa Danny Danon amesema nchi hiyo haina nia ya kuutanua mzozo katika eneo la Mashariki ya Kati lakini haitaruhusu kundi la Hezbollah kuendelea na uchokozi wake.