Urusi imetangaza kuviteka vijiji vingine viwili Ukraine
3 Desemba 2024Matangazo
Jeshi hilo la Urusi limeandika kwenye ukurasa wa Telegram, kwamba vikosi vyake vimetwaa udhibiti wa kijiji cha Novodarivka kilichoko Kusini mwa mkoa wa Zaporizhizhia na cha Romanivka kilichoko mkoa wa mashariki wa Donetsk.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz azuru Ukraine na kuahidi msaada zaidi wa kijeshi
Kadhalika Urusi imeshambulia miundo mbinu ya nishati ya Ukraine kwa droni za kijeshi usiku wa kuamkia leo katika mji wa Ternopil ambako mtu mmoja ameuwawa na wanne kujeruhiwa.
Kwa upande wake Ukraine imesema vikosi vyake vilizuia juhudi za Urusi kuvuka mto Oskil kuingia Kaskazini Mashariki mwa Ukraine.