1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaendeleza mashambulizi mashariki mwa Ukraine

24 Novemba 2023

Vikosi vya Urusi vimeendeleza mashambulizi katika mji wa mashariki mwa Ukraine wa Avdiivka na kulenga maeneo ya viwanda.

https://p.dw.com/p/4ZOeV
Gari la kijeshi la Ukraine löikirusha kombora kuelekea vilipo vikosi vya Urusi huko Donetsk.
Gari la kijeshi la Ukraine löikirusha kombora kuelekea vilipo vikosi vya Urusi huko Donetsk.Picha: Diego Herrera Carcedo/Anadolu Agency via picture alliance

Hayo ni kulingana na kiongozi wa mji huo Vitaly Barabash ambaye amesema wamekuwa wakishambuliwa kutoka kila kona na kwa wastani wa mashambulio 30 hadi 40 kwa siku.

Barabash amesema mji wa Avdiivka ambao awali ulikuwa na wakazi 30,000 sasa umesalia na watu wasiozidi 1,350.

Hayo yakiarifiwa, Urusi imesema hii leo kuwa imeharibu ndege 16 zisizo na rubani za Ukraine kwenye rasi ya Crimea na kwenye eneo la mkoa wa Volgograd.

Soma pia:Urusi yadai Ukraine ilijaribu kuishambulia Kremlin, Kyiv yakanusha

Wakati huo huo jeshi la Ukraine limesema mifumo yake ya ulinzi wa anga imedungua usiku wa kuamkia leo, ndege tatu zisizo na rubani zilizotengenezwa na Iran na kurushwa na vikosi vya Urusi.