1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yaendeleza mashambulizi nchini Ukraine

18 Mei 2024

Urusi imeendeleza mashambulizi katika eneo la kaskazini mashariki mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4g1NH
Mashambulizi ya Urusi huko Kharkiv nchini Ukraine
Uharibifu ulioshuhudiwa baada ya mashambulizi ya Urusi huko KharkivPicha: Anadolu/picture alliance

Lakini Rais wa Urusi Vladimir Putin aliye ziarani nchini China amesema nchi yake haina mpango wa kuudhibiti mji muhimu wa Kharkiv, lakini wanalenga kuunda eneo la kiusalama kwa nia ya kuilinda Urusi.

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema hii leo kuwa shambulio la ardhini lililoanzishwa na Moscow wiki iliyopita katika eneo la Kharkiv linaweza kuashiria hatua ya kwanza ya Urusi katika mashambulizi mengine zaidi, na kusema wanahitaji ndege za kivita 100 ili kukabiliana na Urusi.

Soma pia: Putin: Hakuna mpango kuukamata mji wa Kharkiv kwa sasa

Kulingana na takwimu iliyotolewa na Taasisi ya Utafiti wa masuala ya Vita (ISW), kati ya Mei 9 na 15 mwaka huu, vikosi vya Urusi vimefanikiwa kuchukua udhibiti wa karibu kilomita 278 za mraba, ikiwa ni mafanikio yao makubwa zaidi katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu.