1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yatumia droni 28 kuishambulia Ukraine

11 Julai 2023

Jeshi la Ukraine limesema Urusi imefanya mashambulizi ya droni 28 aina ya Kamikaze kwenye bandari ya Odesa na mji mkuu Kyiv masaa chache tu kabla ya kuanza kwa mkutano wa kilele wa NATO nchini Lithuania.

https://p.dw.com/p/4TimW
Vostok 2018 military exercise in Transbaikal Territory, Russia
Picha: Vadim Savitsky/TASS/dpa/picture alliance

Jeshi la anga la Ukraine limeeleza kuwa mifumo yake ya ulinzi imefanikiwa kuzuia droni 26 zilizotengenezwa na Iran maarufu kama Shahed wakati huko Odesa, droni nyengine 22 ziliangushwa japo mbili zililenga jengo moja ndani ya bandari hiyo.

Soma zaidi: Droni ya Marekani yaanguka baharini, Urusi yaombwa maelezo

Gavana wa Odessa, Oleh Kipeh, ameandika kwenye mtandao wake wa Telegram kuwa ghala la kuhifadhi nafaka na sehemu moja iliyoko karibu na bandari ilichomeka japo hakukuwa na ripoti yoyote ya uharibifu mkubwa au majeraha.

Jeshi la Ukraine limeongeza kuwa, mashambulizi yote ya droni yaliyolekezwa Kyiv yalizuiwa.