Niger yakubali pendekezo la Algeria kuwa mpatanishi
2 Oktoba 2023Hatua hii inafikiwa wiki tano baada ya taifa hilo la Kaskazini kwa Afrika kupendekeza kipindi cha mpito cha miezi sita nchini Niger kitakachoongozwa na raia.
Wizara hiyo imesema imepokea idhini rasmi ya ombi la rais Abdelmajid Tebboune wa Algeria la kutaka kuwa mpatanishi. Hadi sasa utawala wa kijeshi wa Niger haujatoa tamko lolote juu ya hatua hiyo.
Algeria mara kwa mara imeonya kuhusu hatua ya uingiliaji kijeshi Niger ambako jeshi lilimpindua rais Mohammed Bazoum mwezi Julai likipendekeza kuwepo miaka mitatu ya kipindi cha mpito.
Mwishoni mwa mwezi Agosti, Waziri wa mambo ya nje wa Algeria Ahmed Attaf alisema taifa hilo limezungumza mara kadhaa na utawala wa kijeshi wa Niger na kupendekeza mkakati wa kuirejesha nchi hiyo katika utawala wa kikatiba.