Uturuki kufanya kura ya maoni ya katiba
12 Septemba 2010Lengo la shughuli hiyo nzima ni kufanya mageuzi katika mahakama isiyofuata mitazamo ya kidini inayotofautiana na uongozi unaoegemea Uislamu wa Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan.Mageuzi hayo kadhalika yana azma ya kuyapunguza madaraka ya jeshi la nchi hiyo ambalo pia mtazamo wake hauegemei misingi ya kidini.Kulingana na kura za maoni,watu wachache wanayaunga mkono mabadiliko hayo yatakayofanyiwa ibara 26 ili kuiwezesha katiba kuzifuata taratibu za Umoja wa Ulaya.
Kwa mujibu wa wakosoaji,azma ya chama tawala cha AK cha Waziri Mkuu Erdogan ni kuuondoa mfumo wa nchi hiyo usiofuata misingi ya kidini.Wanasiasa wengi wa vyama vya upinzani wamewatolea wito wafuasi wao kupiga kura ya kutoyaidhinisha mabadiliko hayo nacho chama kikuu cha Wakurdi kimetowa wito wa kususiwa kwa kura hiyo.