Uturuki kuzungumza na Instagram baada ya kuifungia
5 Agosti 2024Waziri wa Uchukuzi na Miundombinu wa Uturuki, Abdulkadir Uraloglu, alisema siku ya Jumatatu (Agosti 5) kuwa mazungumzo hayo yangelifanyika baada ya afisa mmoja mwandamizi wa Uturuki kuushtumu mtandao wa Instagram kwa kuzuia machapisho ya rambirambi kufuatia mauaji ya kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Uturuki, Fahrettin Altun, wiki iliyopita aliikosoa Instagram kwa kuzuia baadhi ya machapisho kwenye mtandao huo.
Soma zaidi: Hofu yaongezeka kuhusu kutanuka kwa mzozo kati ya Israel na Hezbollah
Msemaji wa kampuni ya Meta inayomiliki mtandao wa Instagram alisema walikuwa wanafanya kila liwezekanalo kurejesha hali ya upatikanaji wa kawaida ya mtandao huo.
Uturuki inashikilia nafasi ya tano duniani kote kwa kuwa na watumiaji wengi wa mtandao wa Instagram.
Nchi hiyo ya Eurasia ina zaidi ya watumiaji milioni 57 ikitanguliwa na India, Marekani, Brazil na Indonesia.