1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Venezuela yawazuia raia 7 wa kigeni kwa njama ya kumuua Rais

18 Septemba 2024

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Venezuela, Diosdado Cabello amesema wamemkamata raia wa saba wa kigeni nchini humo kwa tuhuma za kula njama juu ya kile ambacho Caracas inadai kuwa ni njama ya kumuua Rais Nicolás Maduro.

https://p.dw.com/p/4kjsW
rais wa Venezuela Nicolas Maduro
Raia saba wa kigeni wanazuiwa nchini Venezuela kwa madai ya kula njama za kumuua Rais Nicolas Maduro Picha: Miraflores Palace/REUTERS

Waziri Cabello ameliambia bunge jana Jumanne kwamba raia huyo wa Marekani "alikamatwa mjini Caracas alipokuwa akichukua picha za mifumo ya umeme, vifaa vya mafuta na vifaa vya kijeshi.

Amesema mshukiwa huyo ambaye hakutambulishwa alikuwa sehemu ya mpango huo dhidi ya Venezuela.

Wiki iliyopita, raia sita wa kigeni - watatu wa Uhispania, Wamarekani wawili na raia mmoja Jamhuri ya Czech, walikamatwa Venezuela kwa tuhuma za kupanga njama za kumuua Maduro, kwa lengo la kuleta vurugu na "kudhoofisha" nchi, amesema Cabello.