Victor Orban ataka Trump kushinda urais Marekani
2 Novemba 2024Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orbán amesema anatarajia Mgombea wa Urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump kuzindua mara moja mpango kwa suluhisho la kidiplomasia kwa vita vya Ukraine ikiwa atashinda uchaguzi wa nchi hiyo mnamo wiki ijayo.
Soma zaidi.Orban: Uchaguzi wa Georgia ulikuwa huru
Orban anayetajwa kuwa mshirika wa karibu wa Trump ameyasema hayo wakati wa hafla ya majadiliano huko mjini Vienna baada ya kuwasiliana kwa simu na Trump na kwamba kutakuwepo na majadiliano ya pamoja na rais wa Urusi Vladmir Putin juu ya kumaliza vita hivyo.
Raia wa Marekani wanapiga kura siku ya Jumanne kumchagua rais mpya. Orbán hajaficha nia yake ya kutaka Trump ashinde kwenye uchaguzi huo dhidi ya dhidi ya mgombea wa chama cha Democrats Kamala Harris.