Vifo vyaongezeka Ukraine kufuatia mashambulizi ya Urusi
29 Desemba 2023Matangazo
Kamanda wa Jeshi la anga la Ukraine Mykola Oleshchuk ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Telegraph kwamba lilikuwa "shambulio kubwa zaidi la anga" tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi huo Februari mwaka jana (2022).
Balozi wa Marekani mjini Kyiv Bridget Brink amesema hii leo kuwa mashambulizi hayo ya Urusi dhidi ya Ukraine yanadhihirisha hitaji la kuipatia ufadhili Ukraine ili kuendelea kupigania uhuru wake.
Soma pia: Watu 24 wauawa Ukraine katika wimbi jipya la mashambulizi
Ikulu ya White House imekuwa ikishinikiza kupata msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine licha ya upinzani mkali kutoka kwenye Baraza la Congress.