Viongozi wa dunia wakusanyika Paris kwa ajili ya Notre-Dame
7 Desemba 2024Viongozi mbalimbali wa dunia akiwemo rais mteule wa Marekani Donald Trump leo wanahudhuria kufunguliwa rasmi tena kwa Kanisa Kuu la Notre-Dame mjini Paris.
Taarifa za ndani zinasema Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewaalika viongozi 50 wa dunia katika ufunguzi wa kanisa hilo ambalo lipo katikati mwa mji mkuu wa Ufaransa wa Paris na ambalo lilichomwa moto wakati wa moto mkubwa mwaka 2019.
Soma zaidi: Macron aapa kusalia madarakani baada ya serikali kuporomoka
Viongozi wengine watakaohudhuria tukio hilo ni pamoja na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen na Rais wa Italia Sergio Mattarella.
Trump alitangaza kuhudhuria tukio hilo siku chache zilizopita kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social na hii itakuwa ni safari yake ya kwanza nje ya Marekani tangu ushindi wake wa uchaguzi mapema mwezi Novemba.