1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Von der Leyen: Chuki dhidi ya Wayahudi haina nafasi Ulaya

30 Oktoba 2023

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amekosoa vitendo vya chuki dhidi ya Wayahudi barani Ulaya vinavyoshuhudiwa katika maandamano na machapisho kwenye mitandao ya kijamii.

https://p.dw.com/p/4YBJa
EU-Kommissionspräsidentin
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der LeyenPicha: Philipp von Ditfurth/dpa/picture alliance

Von der Leyen ameliambia gazeti la Ujerumani la Bild kwamba haifai kuchochea ugaidi na chuki dhidi ya Wayahudi au vurugu dhidi ya jamii ya walio wachache, na kwamba vitendo hivyo havina nafasi barani Ulaya na vinatakiwa kupigwa vita.

Hayo yakijiri, Marekani imelaani leo hii maandamano ya chuki dhidi ya Wayahudi ambayo imesema yanaongezeka kote duniani, baada ya umati wa watu hapo jana kuuvamia uwanja wa ndege wa Dagestan nchini Urusi kufuatia uvumi kwamba kulikuwa na ndege iliyotarajiwa kutua ikitokea Tel Aviv.