Von der Leyen kuizuru Poland kutathmini athari za mafuriko
18 Septemba 2024Matangazo
Poland ni moja ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya katika maeneo ya Mashariki na Ulaya ya Kati yaliyokumbwa na mafuriko tangu juma lililopita.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Czech Petr Fiala, mwenzake wa Slovakia Robert Fico na kansela wa Austria Karl Nehammer wanatarajiwa kukutana katika mkutano wa pamoja na Ursula von der Leyen.
Hayo yanajiri wakati Mji wa mashariki mwa Ujerumani wa Dresden ukiwa katika hatari pia ya kukabiliwa na mafuriko. Kiwango cha maji katika Mto Elbe unaopitia mji huo kimeongezeka na kufikia mita 6 hali iliyoilazimisha serikali kutangaza onyo la pili kubwa la kutokea kwa mafuriko hayo.
Hii inamaanisha maeneo ya makaazi, barabara kuu, na barabara za reli zipo katika hatari hiyo ya kuzidiwa kwa maji.