Waandamanaji Goma, washinikiza kuondolewa kwa MONUSCO
25 Julai 2022Maelfu ya vijana hao waandamanaji waliandamana hii leo katikati mwa mji wa Goma wakitaka kuondoka maramoja kwa ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Congo, Monusco ambao wameda maafisa wake wanakula njama na makundi ya waasi yanayo endelea kuvuruga usalama wa wananchi.
Wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofauti dhidi ya tume hiyo, vijana hao waliingia ndani jengo la Monusco katika mji huu wa Goma na kuliteketeza kwa moto.
Soma zaidi:Mapigano yazuka tena Kongo
Polisi walifafyatua risasi ili kuwatawanya vijana hao ambao walionesha kugoma kutoka katika eneo hilo zilipo ofisi za MONUSCO.
Makundi hayo ya vijana wameiambia DW kwamba wanachotaka ni kuona walinda amani hao wanafungasha virago na kutoka katika taifa hilo.
"Sisi hapa hatupendi MONUSCO sababu wanatutesa watoto na vijana wetu wanateseka sababu ya MONUSCO, wao wanakula vizuri wanalala pazuri hapa waende kwao" mmoja wa waandamanaji aliiambia DW huku akiwa na hasira.
Milio ya risasi yarindima kutawanya waandamanaji
Mchana mzima wa leo jumatatu hali iliendelea kuwa ya wasiwasi katika mji wote wa Goma ambamo mlio wa Risasi uliendelea kusikika nakupelekea kukwama kwa shughuli zote za kibiashara.
Wananchi wakilazimika kubaki majumbani kwao.aidha ,upande wao wanawake kutoka mashirika yakiraia walio anzisha maandamano hayo tangu Wiki iliyopita wameutuhumu ujumbe huo kufuatia kile wanacho kiite uzembe katika utendaji wao kazi kwa zaidiya miaka 20 wakiwa nchini congo.
Soma zaidi:Mvutano kati ya Congo na Rwanda wapamba moto
Katika taarifa yake hapo jana, meya wa mji huu wa Goma Kabeya Makosa alipiga marufuku maandamano hayo, wito uliopingwa na wananchi ambao wameendelea kuzishambulia Kambi za Monusco katika mji wa Goma na wilaya jirani ya nyiragango ambamo waandamanaji walijaribu kuingia ndani ya kamabi ya MONUSCO lakini bila mafanikio .
Haya yanajiri siku chache tu baada ya ujumbe huu kuonesha udhaifu wake katika kukabiliana na kundi la wasi wa M23 waliouteka mji muhimu wa Bunagana huko wilayani rutshuru. Zaidi ya askari (2000 -Elfu mbili) wamekuwa wakihudumu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Wananchi wameendelea kupoteza imani kwa kikosi hicho ambacho wanakishinikiza kuondoka mara moja.Itakumbukwa kuwa wiki iliopita makundi ya wananwake na wanaharakati wa haki za binadamu waliandamana kushinikiza MONUSCO kuondoka katika taifa hilo