Wabunge wa upinzani wavuruga kikao Albania
1 Oktoba 2024Matangazo
Wabunge hao walisema kufungwa kwa Ervin Salianji ni hatua iliyochochewa kisiasa na wameitisha maandamano makubwa ya kuufunga mji mkuu, Tirana, kuanzia wiki ijayo.
Kwa miaka kadhaa sasa, chama cha upinzani cha kihafidhina cha Democratic nchini Albania kimekuwa kikitoa tuhuma kwamba chama tawala cha Kisoshalisti kimeyanyakua kwa nguvu madaraka yote, yakiwemo ya mahakama.
Soma zaidi: Albania yaidhinisha mkataba wa kuwahifadhi wahamiaji
Chama hicho cha upinzani kimekuwa kikiendesha maandamano ya vurugu ya kuipinga serikali tangu mwaka 2013.
Katika tukio la Jumatatu (Septemba 30), wabunge wa chama hicho walimshambulia spika pamoja na mawaziri wa serikali kwa kuwarushia vitu pamoja na kuvitia moto viti.