Wadau wajadili kilimo cha kulinda mazingira mjini Kampala
23 Agosti 2023Kulingana na masharti mapya ya masoko ya kimataifa kuhusiana na bidhaa za kilimo, mazao au bidhaa za mkulima ambavyo vitapandwa kwenye eneo ambako misitu imefyekwa kwa ajili ya kupanua shamba havitakubaliwa katika masoko ya Ulaya.
Tanzania yaanzisha mkakati wa ugawaji ruzuku ya mbolea
Ni kwa ajili hii ndipo mtandao wa Fair Trade ulio na mataifa 29 wanachama kanda ya afrika na mashariki ya kati umo katika harakati za kuwahamasisha wakulima na wadau wote katika mnyonyoro wa uzalishaji kujiepusha na mienendo hiyo ambayo inasemekena ndiyo imesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira hasa pale misitu asili inapofyekwa. AgaPeters Kubasu ni mtratibu wa masuala ya tabianchi katika mtandao wa Fair Trade.
"tumeongea na wakulima kuhusu mabadiliko ambayo yamefanywa na EU. Lazima wazingatie na kuhakikisha kilimo chao kinafanyika katika mazingira ambapo hawaharibu misitu na wanalinda mazingira kwa njia stahiki."
Hata hivyo, kwa mtazamo wa baadhi ya wadau huenda isiwe rahisi kwa wakulima kutii masharti hayo wakati idadi ya watu ikiongezeka kwa kasi barani Afrika huku maeneo ya mashamba yakizidi kupungua kutokana na ukuaji wa miji. Ila kile wanachopendekeza ni vichocheo zaidi kutolewa kwa wakulima ili watumie mbinu na pembejeo za kisasa kuzalisha zaidi kwenye mashamba madogo walio nayo. Wajumbe wawakilishi wa wakulima kwenye kongamano hilo Ressy Mashulano kutoka Kagera Tanzania pamoja na mwenje Njeru kutoka Meru Kenya wamesema.
"Wanakuzuia kukata miti. Mwafrika huwezi kumtenganisha na miti kwa sababu tunaitumia kama nishati,kujenga na katika shughuli zote za kijamii,"
"Sababu iliyokuwa imewafanya wakulima wetu kufa moyo ni bei ya juu ya mbolea. Lakini sasa serikali yetu imerudisha bei hiyo chini."
Wakati huohuo, Fair Trade imeanzisha mkakati wa kuhamashisha wakulima na wadau katika kilimo biashara kufahamu fursa zilizoko kwenye soko huru la Afrika lililozinduliwa mwaka 2021. Kwa sasa ni mataifa 9 tu yamenufaika kutokana na soko hilo kwa kuuza bidhaa zao hasa kwa nchi ya Ghana ambayo masharti yake yamelegezwa ili kuwezesha bidhaa kutoka mataifa mengine ya Afrika kuuzwa katika nchi hiyo. Wajumbe wametoa kauli hizi kuhusu soko huria la afrika maarufu kama AfCFTA.
"AfCFTA ikiweza kutekelezwa tunatumaini kuwa na soko litapanuka na hiyo wakulima wataingiza kipato zaidi kutokana na kiwango cha juu cha mauzo."
"Kazi kubwa ya Fair Trade ni kusimamia ubora na kuusisitiza. Bila kuwa na ubora huwezi kushindana katika soko la kimataifa na hata mataifa ya hapa Afrika"
Wiki ijayo, kongamano lingine la biashara na uwekezaji Afrika Mashariki litafanyika ambapo wajumbe kote mataifa yote ya Afrika watajadili njia za kuchapua shughuli za biashara Afrika kwenye jukwaa hilo la soko huria la Afrika.