1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafugaji wa samaki Kenya wapata hasara ya mamilioni

30 Septemba 2024

Wafugaji wa samaki kwenye Ziwa Viktoria upande wa Kenya wanakadiria hasara ya mamilioni ya fedha baada ya samaki wao kufa usiku wa kuamkia Jumapili.

https://p.dw.com/p/4lEdN
Samaki waliokufa kwenye Mto Xiria nchini Ugiriki.
Samaki waliokufa kwenye Mto Xiria nchini Ugiriki.Picha: Sakis MitrolidisAFP/Getty Images

Inakadiriwa kuwa zaidi ya tani zo za samaki wamekufa kutokana na ukosefu wa hewa safi kwa sababu ya kuchafuka kwa maji ya Ziwa Viktoria. 

Mwenyekiti wa eneo hilo, Joakim Omollo, amesema maji ya ziwa yalianza kubadilika siku kadhaa kabla ya tukio hilo.

Wavuvi wameelezea wasiwasi wao ikizingatiwa kwamba maji hayo yanayotumika pia katika shughuli za nyumbani. 

Soma zaidi: Dhuluma za kimapenzi, ulanguzi wa binadamu na nyinginezo zaongezeka Busia

Maafisa kutoka taasisi ya kitaifa ya utafiti wa bahari na uvuvi kwa ushirikiano na kitengo cha masuala ya uvuvi nchini Kenya wanaendelea uchunguzi kabla ya kutoa ripoti ya kina.

Mara ya mwisho kiasi kikubwa cha samaki kufa katika Ziwa Victoria ilikuwa takribani miaka miwili iliyopita ambapo wavuvi wanaoendesha ufuguaji wa samaki vizimbani katika jimbo la Kisumu na Homabay waliathirika. 

Ripoti ya Wizara ya Uvuvi, Ufugaji wa Samaki na Uchumi wa Majini ilikadiria hasara ya hadi dola milioni 7.2 katika mwaka huo.