Tunapenda sana mazulia ya kiwango cha hali ya juu na yenye kuvutia. Lakini shughuli yake unaijua? Utamaduni mkongwe wa ushonaji mazulia nchini Morocco unakabiliwa na hatari ya kutoweka. Lakini sasa kusini mwa nchi hiyo wanawake ndio wasimamizi wa kazi hiyo ya sanaa na wanajitahidi kuilinda.