SiasaIran
Wagombea urais wa Iran wakabiliana katika mdahalo wa mwisho
3 Julai 2024Matangazo
Wagombea hao walijadili athari za vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani na mataifa mengine ya Magharibi na kuwasilisha mipango yao kuhusu kufufua mkataba wa nyuklia na mataifa yenye nguvu duniani.
Mdahalo huo uliwakutanisha mwanamageuzi asiyejulikana sana Masoud Pezeshkian na mpatanishi wa zamani wa masuala ya nyuklia mwenye msimamo mkali Saeed Jalili.
Soma pia: Raia wa Iran wanapiga kura leo kumchagua rais mpya
Iran itafanya duru ya pili ya uchaguzi wa rais Ijumaa, ikiwa ni mara ya pili tangu Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979.
Ni asilimia 39.9 pekee ya wananchi waliojitokeza kushiriki duru ya kwanza ya uchaguzi wiki iliyopita.